Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Yesu hawezi kutetewa na nguvu za Dola
Serikali, tafuteni sababu nyingine ya kupambana na Waislamu

Na Mwinjilisti Kamara Kusupa

MIMI ninayeandika makala hii ni miongoni mwa maelfu, malaki, mamilioni, mabilioni na matrioli au mazilioni ya wafuasi wa Yesu aitwaye Kristo. Ninaamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwamba alikuja kwamba Yesu alikuwako kabla ya ulimwengu kuumbwa, na kwamba vyote vilifanyika kwa yeye, na baadaye neno alitwaa (alivaa) mwili akakaa kwetu wanadamu akaishi kama binadamu na akashiriki mambo yote yampatayo binadamu aliyepata kuishi dunia hii isipokuwa neno moja tu tofauti na wanadamu wengine yeye Yesu hakuijua dhambi.

Naamini ya kwamba Mungu ni baba yangu, na baba wa wote waliozaliwa upya kiroho na si kwa mapenzi ya mwili, kwaajili hiyo sioni haya kuukiri uungu wa Yesu hadharani nikiungwa mkono na Unabii wa Isaya ambaye alitabiri miaka mingi nyuma akisema: Huku kwetu amezaliwa mtoto mwanaume na jina lake ni: Mshauri wa ajabu. Mungu mwenye nguvu na Baba wa Milele. Yeye ambaye uweza wa kifalme u mabegani mwake. Hata hivyo, imani yangu hiyo haiwazuii wala haiwalazimishi Watanzania wengine au Waafrika wengine ama wanadamu wengine kuamini vinginevyo.

Wapo wanaoamini kwamba Yesu alikuwa Nabii tu wa Mungu, na wala si mwana wa Mungu, wapo wanaoamini kwamba Yesu hakuwa nabii bali alikuwa ni mwanadamu mwenye vipawa au "Charismatic Person" na pia wapo wanaoamini kwamba kitu kiitwacho Mungu hakuna. Wakomunisti kabla ya dini yao kuanguka walikuwa wakikiri hadharani kwamba Mungu siyo Mungu bali Mungu ni hakuna (opium) na kutokana na imani yao hiyo hakuna aliyewabughudhi kwamba wanakashifu dini za watu wengine waaminio kwamba Mungu yuko na ambaye yuko wala hakuna aliyewafunga kwa kuikiri imani yao hiyo hadharani. Maana ukweli na uhalisi wa mambo ni kwamba hicho ndicho kitendawili cha imani hakina jibu moja na dhehebu moja na Doctrine moja kitu ambacho hakitatokea asilani badala yake kinachotakiwa sasa ni sote tusubiri kwa uvumilivu mkuu hadi siku ya kiama ambayo ndiyo siku ya kuteguliwa kwa kitendawili cha imani, hapo tukapoona Mungu mwenyewe akiwalipa wanadamu kwa kadri ya imani zao na matendo yao.

Sasa muda wote tuwapo duniani hatuna budi kukubali kutofautiana na pia kukubali kutokubaliana. Ni kwa misingi hiyo ya kukubali kutofautiana ndiyo maana imani yangu hainizuii kuishi na Waislamu, kushirikiana nao katika mema, na hata kutumia magazeti yao ya kidini ambayo lengo na madhumuni ya kuweko kwayo ni kueneza Uislamu, kuutetea na kuuimarisha pale ulipolegea. Imani yangu haiwafanyi wale wanaoamini kinyume nami wawe maadui zangu, wala haiwafanyi Waislamu na wengine wanaoamini kwamba Yesu siyo Mungu, Yesu siyo Nabii au siyo mwana wa Mungu wawaone Wakristo kama maadui zao.

Katika nchi hii kama ungekuwako uadui wowote kati ya Wakristo na waumini wa dini nyingine, ama uadui kati ya Waislamu na wasio Waislamu, badi uadui huo ungeonekana maishani tangu enzi za mkoloni, hadi uhuru, hadi sasa. Kwa ajili hiyo lililo wazi ni kwamba mapambano yanayoendelea sasa kati ya Waislamu na serikali, hayatokani na imani yaani eti Waislamu wawe wanaamini tofauti na Wakristo wanavyoamini, ama Wakristo kuamini tofauti na wanavyoamini Waislamu kwani tofauti za imani zilikuwepo tangu mwanzo na zitaendelea kuwako hadi siku ya mwisho Mungu mwenyewe atakaposimamisha ufalme wake wa milele.

Sasa swali la kujiuliza kwa dhati ni hili, ni nini hasa kinachopelekea watu kufungwa ama kuwekwa mahabusu na kunyimwa dhamana? Narudia tena kukanusha kwamba imani kama ilivyo haiwezi kuwa chanzo cha vurugu au mapambano ni lazima kuna sababu nyingine iliyojificha nyuma yake. Binafsi naagizwa na maandiko yaliyoko kwenye Biblia kwamba tuishindanie imani tuliyopewa mara moja tu. Hii ina maana ya kwamba wakati wa mahala pa kuishindania ama kuipigania imani ya Kikristo ni duniani tu tena ni mara moja tu yaani katika atakuwa hana nafasi tena ya kuitetea imani au kigharamikia kwa namna yoyote. Lakini pia mafundisho ya Biblia yanaonya kwamba kushindana kwetu sisi au vita vyetu si juu ya nyama na damu, bali ni juu ya falme, na mamlaka na Roho wachafu katika ulimwengu wa roho. Ninachotaka kieleweke katika mada hii ni kwamba imani ya Kikristo kamwe haiwezi kutetewa na nguvu za dola, vinginevyo Yesu kama mwasisi wa imani yetu atakuwa hana cha kujivunia.

Wale wamwaminiao Yesu wataitetea imani yao kwa kutiwa nguvu na Yesu mwenyewe badala ya nguvu za dola ambazo wakati mwingine hutumika kuonea zaidi kuliko kutenda haki. Katika neno hili serikali isiufanye ukiri wa Wakristo kwamba Yesu ni Mungu mwenye nguvu iwe kisingizio cha wao kupambana na Waislamu, maana ukweli wa mambo ni kwamba Yesu kuaminiwa kama Mungu ama kuaminiwa kama Nabii tu hizo ni doctrine siyo issues za kuvuruga jamii ama kuitikisa misingi ya umoja na mshikamano wa nchi. Tatizo halisi ni kwamba serikali ya CCM ina chuki zake tena za muda mrefu dhidi ya Waislamu kwa sababu Waislamu wamekuwa wakiipinga wazi wazi kwa vile wao Waislamu dini yao inaruhusu wao kujihusisha na siasa.

Ni kutokana na upinzani huo ndiyo maana serikali ya CCM siku zote imekuwa na approach za ukali na ukatili unaoandamana na matumizi ya ziada ya nguvu za dola hata pale mahala pasipostahili kutumia nguvu za dola. Serikali ina chuki zake kwa Waislamu kwa sababu wanaipinga na si kwa sababu Waislamu wanampinga Yesu kwa kusema Yesu si Mungu. Kama huu ndiyo uhalisi wa mambo, basi nasema serikali itafute kisingizio kingine cha kupambana na watu inaowachukia, isitumie mgongo wa Ukristo kwani inajulikana wazi kwamba serikali yetu haimuenzi Mungu, wala haimuenzi Kristo badala yake inaenzi uchawi na ushirikina. Serikali iwayo yote haiwezi ikawa na huruma kwa Mungu lakini ikakosa huruma kwa raia zake, haiwezekani kabisa serikali ikamhurumia Mungu asiyeonekana, ama ikamhurumia Yesu ati anakashifiwa na Waislamu wanaosema Yesu si Mungu lakini wakati huo huo serikali hiyo ikakosa huruma kwa raia zake wanaoonekana ikawakomoa kwa kuwashitaki eti wameandamana na papo hapo kuwanyima dhmana ambayo ni haki yao ya kisheria! Yesu anao uwezo wa kuwainua watu miongoni mwa wale wamwaminiao, nao wakamtetea kwa hoja, kwa matendo ya miujiza na mahubiri yenye mvuto. Kwa ajili hiyo mapambano kati ya serikali na Waislamu yasinasibishwe na Ukristo kwa namna yoyote kwa kuwa ni mapambano ya kupigania na kuhami maslahi ya kidunia wakati ufalme wa Yesu siyo ufalme wa maslahi. Zaidi ya yote Muislamu anapoandamana na kusema wazi kwamba Yesu siyo Mungu, lugha ya namna hiyo haimpunguzii chochote Yesu katika ukamilifu wake. Maneno ya kwamba Yesu si Mungu hayamuondolei Yesu Uungu wake wala hayamfanyi asiwe Mungu, sawa kabisa na ukiri wa Wakomunisti wa kusema Mungu hayuko ambavyo haukumfanya Mungu aache kuwa.

Pia katika sakata hili la kuukana Uungu wa Yesu popote pale litakapoibukia Yesu mwenyewe atajipigania na kujitukuza kwa njia zake za kimungu na siyo za kidola. Na sasa tulitazame suala la maandamano, je kuandamana kama kulivyo kuna kosa gani? Kama Waislamu waliumizwa na hukumu dhidi ya Muislamu mwenzao aliyefungwa kwa kusema Yesu siyo Mungu kuna ubaya gani wa wao kuandamana na kuzieleza hisia zao kwa amani? Mbona mashoga wa Ulaya walimfanyia maandamano Rais Mugabe wa Zimbabwe kupinga misimamo ya serikali yake dhidi ya mashoga wenzao waishio Zimbabwe!! Kwa hiyo tatizo hapa ni ile kasumba ya Kikomunisti ya CCM ya kuona maandamano yoyote yasiyokuwa ya kibali cha serikali ni haramu na kwa sababu wao watawala wanayaona haramu hata mwandamanaji wanamwona kama ni mtu haramu ambaye hana thamani wala haki ya kuishi ndiyo maana wanasema na kuandika bila haya Muislamu aliyekatwa mguu ajutia kitendo chake cha kuandamana, kisa! Asema shs 2000 zilimponza.

Ni nani anayeweza kuhonga waandamanaji ili waelezee hisia zao? Kisha hata tukiichukulia hali hiyo iwe kweli kuwa mwandanamaji kahongwa shilingi 2000, je wewe unayemrushia bomu au silaha ya kumkata mguu maskini huyu una nini cha kujivunia katika utawala wako? Je waweza kuthubutu kujidai kwamba unao askari wakali sana kwa kuwa wanaweza kuwavunja miguu raia zako na kuwanyamazisha wasiandamane!! Ukweli na uhalisi wa mambo ni kwamba hizi ndiyo ishara na dalili za mwisho za serikali iliyoshindwa kazi. Maandamano mengi tunayoyaona leo yana uhusiano wa moja kwa moja na uchaguzi mkuu wa 2000. Wakati wa uchaguzi mkuu CCM ilitumia fedha nyingi sana ambazo haijulikani chanzo chake, matokeo yake ni kwamba baada ya uchaguzi imebidi serikali ifidie gharama za uchaguzi kwa njia ya kuminya kutoka kwenye huduma za jamii na mafungu ya maendeleo social services zimekufa na hizo zilizo hai zinazidi kudidimia siku baada ya siku, ajira haiongezeki na wasio na kazi wala shughuli maalum za kufanya wanazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Haya ni matatizo ya kijamii (siyo matatizo ya imani) na ni wazi kwamba yana uhusiano na kutawala ulioshindwa kazi (umeshinda kwenye kura kwa kishindo lakini pia kwenye kazi umeshindwa kwa kishindo). Hivyo basi waandamanaji ni lazima waionyoshee kidole CCM kwa sababu ndiyo iliyokomba fedha yao wakati wa uchaguzi, fedha ambayo ilipaswa kuwaboreshea maisha lakini ikamwagwa kwenye mabango ya chagua Mkapa na picha mamilioni ambazo sasa zimesimama kama kejeli tu zikiwa na ujumbe ule ule Chagua Mkapa, Chagua CCM. Mtu asije kushangaa kwamba leo hii vyombo vya habari vinatangaza na kuandika juu ya ofisi za CCM kuchomwa moto baada ya maandamano ya Waislamu lakini kama atajitokeza mtu mmoja kisha akasema anaitisha maandamano ya kujibu kwamba Yesu ni Mungu, si ajabu waandamanaji wakawa wale wale na ofisi za CCM au vituo vya polisi vikachomwa moto.

Kwa hiyo siyo halali kuhusisha ulipuaji wa mabomu, au kuchomwa moto ofisi za CCM na Uislamu, ieleweke wazi kwamba katika nchi hii kuna Waislamu, Wakristo, Wahindu ambao wanayo haki ya kuelezea hisia zao na pia kuna dhehebu moja liitwalo dhehebu la Ulalahoi, hawa walalahoi wana uchungu usiokwisha na jeraha mioyoni mwao lisilopona kutokana na ukweli kwamba wamenyimwa kula mema ya nchi yao, hawa wanangoja itokee nafasi yoyote japo ya muda mfupi tu ili waonyeshe hisia zao. Sasa nasema ole wenu ninyi mlioiibia nchi mkajenga mahekalu yenu huko maeneo ya vigogo na wengine mkaficha fedha kwenye mabenki ya Ulaya!! Ole wenu mlotumia mabilioni kama gharama ya kuingia madarakani dhambi hiyo mliyoitenda itawatesa daima kwani sasa itabidi nanyi mzilipe gharama za kuweko madarakani.

Vita ya Kidini Tanzania?!!!

 

 

Matatizo yanayopikwa Tanzania sasa hivi yana michango mingi iliyochangia kuyafikisha hapo yalipo,Lakini Nyerere pamoja na kwamba ni marehemu hawezi kuepuka lawama.Aliitawala Tanzania kama mali yake, na mawazo yake ndiyo yaliyokuwa sahihi, Na hata kama aliweka Mtu, alihakikisha ni mjinga atakayeketi miguuni pake siku zote kufundishwa.

Namkumbuka Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye Nyerere alifikiri ni mjinga, lakini baada ya kutawazwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano, alianza kufanya vitu vyake kama mwanaume anayefikiri. jambo ambalo lilimletea mikwaruzo na huyo aliyekuwa akijifanya kujua kila kitu.

Kwa sasa kuna Mkapa anayeitwa Rais wa Tanzania, Lakini nikienda Tanzania nitakutana na mzee Ali Hassan Mwinyi kwani kwangu huyo ndiye mtu aliyethubutu kuwa na mawazo huru wakati wa Nyerere kwenye uongozi wa Nyerere. Mkapa na wenzake wanatakiwa wajue kuwa sasa Nyerere hayuko, na majukumu ya kuiongoza Tanzania lazima yahusishe Watanzania wote.

Kiburi kwamba wao ndio walioachiwa nchi waache. Hata huyo wanaedai kuwa aliwaachia Tanzania haikuwa yake. Matatizo ya Zanzibar yatafutiwe uvumbuzi wa haraka unaozingatia haki na siyo ubabe kama serikali inavyojaribu kufanya.

Madai ya chama cha CUF kwamba uchaguzi urudiwe na iundwe tume huru, pamoja na kubadilishwa kwa katiba yatiliwe maanani kuinusuru nchi na vita vya kidini ambavyo vinaonyesha kila dalili ya kuanza. Wakristo wasifurahi kwamba serikali ya Mkapa inawazibiti Waislamu, wajue kuwa serikali hiyo hiyo inaweza ikawageukia na wao.

Mkapa aache mara moja kuitegemea Amerika kumsadia kutatua tatizo la Tanzania kwani sera za Marekani ni kuwanyanyasa Waislamu duniani kote.Wananchi wa Tanzania wana uhuru wa kuamini dini yeyote na ikiwa Wazanzibar wengi ni waislamu sioni sababu ya wao kuadhibiwa kwa sababu ya dini wanayoiamini.

Hata kama wanataka kuuvunja muungano kwa sababu wanazozijua wao, wawe huru kufanya hivyo kwani ni kinyume kuwalazimisha kubaki kwenye muungano ambao hawaoni faida yake.

Nyerere alipata sifa duniani kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, na Mkapa atapata sifa ya kutenganisha Zanzibar na Tanganyika kuepusha umwagikaji wa damu. Kila kitu kina wakati wake. Wakati wa Nyerere ulikuwa wa kuunganisha, siyo vibaya wakati wa Mkapa ukawa ni wa kutenganisha kwa faida ya walio wengi.

Kumuenzi Nyerere siyo kumwaga damu kutetea sera zake ambazo alizitetea bila kumwaga damu.

Mwisho ni vizuri Mkapa akajua kwamba yeye siyo Nyerere, na kuna vitu alivyoviweza Nyerere ambavyo yeye haviwezi. Pia asisahau kuwa kizazi alichokitawala Nyerere ni tofauti kabisa na kizazi anachokiongoza.

Sura nzuri na maumbile ya Nyerere yalimsaidia kusamehewa haraka na umma, Wakati sura ya kutisha na maumbile ya ajabu ya Mkapa yanamfanya awe mtu asiyesamehewa haraka akikosa.

Tayari Mkapa ameshaukosea umma wa Watanzania kwa kuamuru Polisi wawaue zaidi ya watu hamsini huko Zanzibar, sijui itawachukua muda gani kumsamehe. Lakini kama ningekuwa Mkapa, Ningejiuzulu niombe msamaha, halafu niruhusu jeshi lichukue uongozi kwa muda, na baadaye limkabidhi Kijana Faustin Munishi madaraka

Nchi ya Tanzania ni mali ya watanzania wote na siyo ya Mkapa na CCM kama inavyoekea kuwa.Vitendo vinavyofanywa na serikali ya chama tawala CCM vinaonyesha wazi jinsi wanavyofikiri kuwa Tanzania ni mali yao.

Kwamba serikali inaweza kuwaua raia wake kwa sababu wana mawazo yanayotofautiana na chama tawala, siyo tu ni kinyume na haki za binadamu, bali ni wendawazimu uliochanganyika na upumbavu wa hali ya juu.

Nauita upumbavu kwa sababu ni afadhali ungekuwa ujinga ambao unaweza kutoka wakati mhusika anapoelimishwa. Lakini kwa kuwa yalifanywa na watu wanaojiita wasomi tena wa vyuo vikuu, basi yanakuwa ya kipumbavu maana hatujui wahusika wataenda chuo gani tena kuelimika ili wajue kuwa katika dunia tunayoishi ni vigumu watu wote kukubaliana kimawazo, hata kama mawazo hayo yanatoka kwa Rais wa nchi.

Matata na chokochoko zilizoko duniani mara nyingi huanzishwa na watu wanaojifanya kujua kila kitu, na kumbe hawajui kwamba hawajui. Na Tanzania tuna Mkapa anayejifanya kujua kila kitu na kumbe hajui impasavyo kujua. Matokeo yake ni kwamba Tanzania itaigizwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havijawahi kuonekana popote duniani.

Nasema itakuwa vita mbaya kwa sababu karibu kila mtu Tanzania amepitia mafunzo ya kijeshi, kosa alilolifanya Nyerere akifikiri kila mtu anapokuwa mwanajeshi ni rahisi kumtawala mtu huyo.

Jeshini hawaulizi maswali, bali wanatii amri. Ni kigezo hicho ndicho kilichomfanya Nyerere aamini kuwa watanzania wakipata mafunzo ya kijeshi watakuwa na nidhamu, na itakuwa rahisi kuwatawala. Alifanikiwa kuwatawala watanzania kwa karibu miongo miwili bila ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Siyo kwamba Tanzania haikuwa na matatizo, lakini alijua nini cha kufanya yanapojitokeza tofauti na anavyofanya Mkapa ambaye anafikiri kila tatizo linatatuliwa kibabe na kutumia nguvu za dola.

Watanzania aliowatawala Nyerere ni wale wale Mkapa anaoshindwa kuwatawala, tofauti ni kwamba Nyerere aliweza kuwaibia watanzania bila wao kujua, wakati Mkapa anawaibia waziwazi. Nyerere alikuwa akigundua wananchi wamemshtukia anawaomba msamaha wa geresha wakati mkapa anamwamuru mkuu wa Polisi awashughulikie wote wanaokuwa na mawazo tofauti na chama tawala. Nao Polisi kama 'Robots' na bila kutumia ubongo wao wanawamiminia risasi za moto ndugu na dada zao watanzania na kusababisha vifo ambavyo idadi yao haitajulikana kamwe. Serikali inasema ni watu 23 tu, wakati chama cha upinzanini CUF ambacho ndicho kilichoadhirika kwa wanachama wake kuuawa kinasema watu zaidi ya 300 waliuawa kinyama na mamia kujeruhiwa huku maelfu wakiwa wakimbizi wa kisiasa Mombasa Kenya kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru. Na yote hayo yamesababishwa na utawala wa kimabavu wa dikteta Mkapa.

Kinachoshangaza na kogopesha siyo idadi ya watu waliokufa, bali tumefikia mahali ambapo Polisi wa Tanzania wanatumia bunduki zilizonunuliwa na watanzania kuwaua watanzania. Mbaya zaidi ni kwamba karibu watanzania wote waliokufa dini yao ni ya Kiislamu jambo linalolielekeza tatizo lenyewe kuwa la kidini zaidi kuliko kisiasa. Siyo kwamba likiwa la kisiasa pekee ni rahisi kulitatua, maana sidhani Tanzania ya leo kuna mwanasiasa anayejua siasa za kutosha kulitatua. Mkapa ni mtoto asiyekua kisiasa na siyo makosa yake.

Nyerere baba yake kisiasa hakutaka akue ili awe anamnywesha maziwa ya kisiasa kila siku. Alifikiri angekuwepo mpaka azaliwe mtoto mwingine ambaye naye kama Mkapa, mpango ulikuwa kwamba asiruhusiwe kukua bali aendelee kupewa maziwa ya kisiasa sijui ingekuwa mpaka lini.

Lakini alisahau kuwa mwanadamu hawezi kuishi milele duniani, ila mbinguni au motoni ndiko watu wanakoishi milele.

Mungu alipoamua kumchuku Nyerere {na sijui alimweka wapi,}Ndipo mambo yalipoanza kumharibikia Mkapa. Kama mtoto yatima kisiasa, hakujua aanzie wapi amalizie wapi. Ninasikitika kusema kuwa mpaka sasa Mkapa amechanganyikiwa kisiasa. Wanaojifanya kumshauri ndio wanaoharibu zaidi. Inavyoonekana hatujui ni nani hasa anaeiongoza Tanzania kati ya Mboma mkuu wa majeshi, Maita mkuu wa Polisi, na Kingunge Nguoyambali Mwiru mshauri mkuu wa Mkapa.

Habari kutoka vianzio vyetu zinasema kuna uvutano mkubwa kati hawa watatu kila mmoja akidai kuachiwa urithi wa Tanzania. Mboma anadai kuwa Nyerere alimwambia alinde muungano kwa nguvu zote na akiona kuna hatari ya muungano kuvunjika, Jeshi lichukue madaraka. Kingunge naye anadai kuwa Nyerere alimwambia atumie busara yote kuhakikisha siasa zinaendeshwa bila kumwaga damu ya Watanzania. Naye mkuu wa Polisi anadai kuwa Nyerere alimwambia awafuatilie kwa karibu wanasiasa kuhakikisha kuwa hawaiuzi nchi kwa mabepari wa mataifa ya magharibi. Mkapa naye anadai kuwa Yeye ndiye aliyeachiwa nchi kuhakikisha kuwa siasa ya ujamaa haifutiki Tanzania.

Ukiyaangalia madai yao, na uwe kidogo ulimfahamu Nyerere, utakubaliana nao kuwa wote wanasema ukweli. Ni ukweli kwa sababu mwalimu alitaka kuwaona kila siku Butiama wakilalamika kwaba hili halitekelezeki kwa sababu linapingwa na lile. Yaani alihakikisha kuwa la mkapa halitekelezeki kwa sababu linapingwa na Mkuu wa Polisi. Na lile la Mkuu wa majeshi linakwamishwa na KINGUNGE NGUOYAMBALI.

Wakati kila mmoja wao alipopeleka malalamiko yake Butiama ndipo Nyerere alipata nafasi ya kuwaonyesha jinsi walivyo wajinga, na inasemekana alikuwa akiwafundisha kama watoto wa Nasari. Ndio maana wote wanamwita mwalimu. Ni kweli alikuwa mwalimu wao.

Sasa Mwalimu hayupo, na wanafunzi wake wameanza kuvurunda mambo.Tayari Polisi wamewaua raia zaidi ya 50 wasiyo na hatia kwa madai kuwa walihudhuria mkutano wa kuda haki yao waliyonyanganywa na Serikali.

Ni baada ya mauaji hayo ndipo Watanzania wameanza kuhoji hivi Tanzania ni ya nani hasa?

Wanajiona kama hawana haki ya kudai chochote katika nchi yao.Wakitafuta wa kulaumu wanamuona Nyerere waliyemwita BABA.

Wanaona Nyerere alikosea kuwaachia urithi watu wanne tu na kuwasahau watu milioni karibu 40 kutegemea maamuzi ya watu wanne.

 

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>