Redio ni nyenzo muhimu ya kuhubiria injili ya Yesu mwokozi. makanisa
yakiitumia vizuri inaweza kuwarahisishia kazi yao. Kwa hiyo ni
muhimu kwa makanisa kutilia maanani matumizi ya redio kama chombo
cha kuipeleka habari njema kwa watu wote. Na itakuwa rahisi zaidi
ikiwa makanisa husika yatamiliki redio zao ili kuokoa gharama.
Nayapongeza
makanisa ambayo tayari yameuona umuhimu huo, na yanaendesha vipindi
vya kiinjili katika redio za kibiashara zilizopo.
Ni
muhimu kuanzisha redio za injili ili kuzitumia kuhubiri habari
njema. Dunia inabadilika haraka na kanisa lisipokwenda na wakati
litaachwa mbali kimawasilino. Pamoja na kuanzisha redio ni muhimu
kujua kutumia vyombo vya mawasiliano kwa ujumla kuepuka makosa
yanayofanywa na wahubiri wa TV. na redio. Wanatumia vipaza sauti,
na bado wanapayuka kwa sauti ya juu kiasi cha kuharimu makoo yao
na masikio ya wasikilizaji wao.Umewahi kumsikia Lai , Mark Kariuki
na Muiru? Utajaza mwenyewe.