Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Munishi siyo mwanasiasa


"Mimi siyo mwanasiasa na sitarajii kuwa mmoja wao"

Lengo kubwa kwenye makala yangu halikuwa kumkosoa Nyerere tu, ila kuwatahadharisha akina Mkapa na CCM kwa ujumla kuhusu hatari ya kuendeleza makosa ya Nyerere. Kwao Nyerere hakuwa na kosa, na kila alichofikiri kinatakiwa kidumu.

Nyerere kama walivyo wanadamu wengine, alikuwa na makosa kibao. Na kusema zidumu fikra za marehemu ina maana ya kudumisha makosa yake. Pengine wangekuwa na hekima wangesema," Zidumu fikra chache za mwalimu, na zile mbaya kama za ujamaa zizikwe pamoja naye.

Lakini kwa mtazamo wangu sioni kuna haja ya kudumisha fikra zozote za marehemu kwani kuna walio hai wanaofikiri kuliko Kambarage. Nina haki ya kuamini hivyo bila kumzuia yeyote kuamini vinginevyo, kwani uhuru wangu wa kuamini kuwa Nyerere alikuwa MPUMBAVU unaishia pale uhuru wa mwingine kuamini alikuwa Mwerevu unapoanzia.

Ila sidhani kwamba baada ya kuifanya Tanzania maskini kwa sera zake mbovu za ujamaa, kuna mtu mwenye akili timamu atakayesema Nyerere alikuwa bora kuliko Idd Amin wa uganda. Nyerere aliua watu wengi kwa njaa na magonjwa kuliko Idd Amin.

Lakini watu hawakumwamini Amin kwa sababu aliua akitumia bunduki. Madhara ya Amin uganda yalimalizika japo yuko hai, lakini madhara ya Nyerere Tanzania yanaendelea akiwa kaburini.

Wanaposema wakati wa Mwinyi na Mkapa vyombo vya dola vinawaua wananchi wasio na hatia kuliko wakati wa Nyerere nawashangaa!!!!! Wanasahau kuwa Mwinyi na Mkapa waliteuliwa na Nyerere. Tanzania hatujawahi kuwa na wakati wa kiongozi mwingine isipokuwa Nyerere. Ndio maana Mungu amenipa mzigo mzito wa kufuta ukiritimba wa mawazo ya Nyerere Tanzania, na kupandikiza mawazo mapya.

Ninaujua ugumu wa kazi hiyo hasa ukitilia maanani kwamba Nyerere alitumia muda wote wa utawala wake kujikita katika nyoyo za watanzania ili wamkumbuke miaka 100 ijayo. Mwaka mmoja tangu afe kwa ugonjwa wa MKANDA WA JESHI{na sijui ni ugonjwa gani huo.}Tayari hisia za watu juu yake zimeanza kubadilika ghafla.

Kwa mbali wameanza kuiona nuru ikiwamulikia na kuwaonyesha kuwa wanaweza bila Nyerere. Wengi wanashindwa kuamini kwamba Tanzania ina watu wenye akili nzuri kuliko Nyerere mara mia moja. Siyo kosa lao, kwani Nyerere aliwataka waamini hivyo. Nikijua wazi kuwa Nyerere aliwanyanganya Watanzania uwezo wa kufikiri, ni juu yangu kuwarudishia uwezo huo ambao ni haki yao kutoka kwa Mungu.

Kinyume na alivyofanya Nyerere nitawaruhusu watanzania wote wafikiri kuhusu hatma ya Tanzania, na baadye kuyatumia mawazo hayo kuiendeleza nchi yetu. Badala ya kupoteza muda mwingi kunilaumu eti nimethubutu kumkosoa Nyerere, tuanze kufikiri jinsi ya kuyatatua matatizo mengi aliyotuachia Nyerere.

Wengine wanasema Nyerere alileta amani Tanzania. Alikuta amani imeenda wapi ndipo akafunga safari ya kwenda kuileta? Eti alituunganisha? Tulivunjwa na nani? Yeye ndiye aliyetuvunjavunja mpaka tukawa hatujui kudai haki zetu za msingi. Sukari sabuni za kuoga na dawa za meno ilikuwa ni bidhaa muhimu kwa kila mwananchi, lakini Nyerere alitufanya tuamini kuwa ni anasa.

Mnakumbuka mwaka 1978 wakati watanzania walipofungwa jela kwa kupatikana na sabuni ya REXONA, COLGATE au mafuta ya kupikia KIMBO kutoka nchi jirani ya Kenya? Huo ndio uliokuwa utawala wa Julias Kambarage Nyerere. Watu walitupa pesa zao baharini kuepuka kuwekwa kizuizini wakiitwa wahujumu wa uchumi.

Pengine mmesahau azimio la Arusha alilotumia Nyerere kuwanyanganya watu mali zao halali na kuzifanya mali za umma. Mashamba na viwanda vyote alivyowanyanganya wawekezaji wa nje na kutaifisha, sasa yako wapi? Yote yameharibika kiasi kwamba hayafai kuitwa mashamba ila mbuga zisizo na wanyama pori.

Viwanda ndio hata usisemme. Vyote vimekufa kabisa. Huo ndio uliokuwa wendawazimu wa yule baadhi ya watanzania wanamwita 'mwalimu' Nitakuwa na kosa gani kama nitamwita Nyerere hayawani aliyekuwa mbinafsi wa mawazo, mtu aliyekuwa na asili ya kimasikini ambaye hakupenda kumwona mtu na kitu chake. Siyo ajabu kwamba alikufa masikini na kuwaacha watanzania wakiwa masikini kuliko yeye mara mia.

Cha ajabu ni kwamba tuna watu wajinga wanaotutaka tumuenzi Nyerere na tudumishe fikra zake za kimasikini. Ikiwa kwa miaka karibu arobaini aliyotawala Nyerere mawazo yake hayakuiendeleza Tanzania, sijui hawa wajinga wanaamini vipi kwamba mawazo hayo yaliyopitwa na wakati yatatuendeleza katika karne hii ya sayansi na teknolojia?

Sina ugomvi na Nyerere maana alimaliza kazi yake na sasa ni marehemu, ugomvi wangu ni kwa hawa walio hai wanaojiita viongozi. Inanipa kichefuchefu ninapomuona Mkapa na vigogo wa CCM wakitoa hotuba zenye maneno ya matisho kwa wale wanaomkosoa mzee wa Butiama.

Ni sawa na mbwa mwitu wanaokula mzoga, na huku wanajaribu kumzuia simba anayejipitia zake kwenda kuwinda. Kwa akili zao ndogo wanafikiri simba anataka kuwanyanganya mzoga uliokufa wenyewe akaugundua fisi kwanza na baada ya kushiba akakaa kando, akiwaeleza jinsi ya kuula huo mzoga.

Kinachonifanya nitake kutapika siyo kuzuiwa kula mzoga, bali Mkapa na wenzake wamepitwa kiakili na mbwa mwitu ninaotaka kuwafananisha nao. Tofauti na akina Mkapa, Mbwa mwitu wakishapata mzoga hawahitaji akili ya aliyewatangulia iwaelekeze waanzie wapi kula. Wanatumia akili kichwani mwao, ambapo Mkapa na wenzake wanatumia akili kutoka kwenye kaburi la Nyerere.

Tanzania kama mzoga ilijifia yenyewe kifo cha kawida kilichokuwa kimeua nchi karibu zote za Afrika. Nyerere kama fisi aliukuta mzoga Tanzania karibu kukata roho na badala aupe huduma ya kwanza akaleta siasa za ujamaa ambazo ziliufanya huo uliokuwa ukionekana kama mzoga kupoteza fahamu.

Nyerere alikula akashiba kutoka mzoga huo, na sasa kina Mkapa na CCM wanakula na wanawatisha kunguru walafi wa nyama yaani akina Mrema Cheyo na Lipumba, wasijaribu kabisa kuusogelea. Sasa simba yaani Munishi anajipitia akiimba nyimbo zake, "CCM imezeeka haifai kuongoza." Mara mbwa mwitu wanaacha kuulinda mzoga wao usiliwe na kunguru, wanakimbia kumzuia simba.

Nani aliwadanganya kwamba mimi ninataka kuwanyanganya mzoga wao? Na kama kweli ninataka wanaweza kunizuia? Nilipoona watu wamekurupuka kuja kunizuia nilijivuta karibu ili nione ni mzoga wa aina gani hawa mbwa mwitu wanajaribu kunizuia na huku nimeshiba baraka za Bwana? Kumbe siyo mzoga ila ni nyumbu alyepoteza fahamu tu na analiwa akiwa mzima. Kuwepo kwangu karibu tu kumewafanya mbwa mwitu {yaani CCM na Mkapa} wakae mbali huku wakikodoa macho. Kunguru nao {yaani akina Mrema cheyo na Lipumba }wanarukaruka juu ya huo uliokuwa ukionekana kama mzoga wakiniomba niondoke ili wajaribu bahati yao.

Nimegundua kuwa huyu nyumbu bado ana uhai, na japo sehemu ya mwili wake imeliwa,bado anaweza kupona. Mungu ndiye alienipa nguvu zinazowafanya wanyama wengine porini waniogope. Nami nitatumia nguvu hizo kumtibu huyu nyumbu mpaka apone. Pia nimegundua kuwa aliyesababisha huyu nyumbu apoteze fahamu ni fisi.{yaani Nyerere} Kazi yangu ni moja. kuhakikisha kuwa nyumbu anapata fahamu na kuweza kujisimamia mwenyewe.

Nitamlinda kutoka kwa hawa wanaotaka kumla akiwa hai. Watanzania Mungu amesikia kilio chenu na ameyaona mateso yenu. Amemtuma Munishi kuwaletea ukombozi. Mbwa mwitu ni kunguru walie tu.

Ameandika Mwinjilisti Munishi

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>