|
|
|
![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Dar
Yatishiwa Kulipuliwa
Na Mwandishi wetu Dar-Es Salaam Wafanyakazi wa CRDB mjini Dar Er Salaam walilazimika kukimbia ofisi baada ya habari kuzagaa kuwa kulikuwa na mabomu ambayo yangelipuka wakati wowote. kulikuwa na pata-shika ya nguo kuchanika wakati kila mtu alipojaribu kutoka nje haraka iwezekanavyo. Wengine hata baada ya kuwa nje hawakujihisi salama, jambo lililowafanya wakimbie bila mwelekeo wa ni wapi hasa walipokuwa wakikimbilia. Hatimaye walifika Polisi ambao nao walikuwa na wasiwasi kama waingie au wasiingie. Waliwatanguliza mbwa ambao baada ya kunusa na kunusa kisha wakanusa tena, walirudi na kuwahakikishia wenzao Polisi binadamu kuwa jengo halikuwa katika hatari yeyote ya kulipuka. Ndipo kwa vishindo Polisi wa Tanzania waliingia ndani na kuanza kupekua kila mahali wakitafuta mabomu. Walipekua halafu wakapekua, na baada ya kupekua wakapekua tena. Baadaye waliwaita waandishi wa habari kutangaza kwamba wataalamu wa mabomu kutoka kikosi cha Polisi Tanzania wamefanya utafiti wao kitaaluma na wamegundua kuwa kulikuwa hakuna bomu lolote katika jengo hilo. Walijigamba kuwa hata kama lingekuwepo na liwe limebakiza sekunde tatu kulipuka, wao walikuwa na uwezo wa kulitegua kininja. Waliwataka wafanyikazi wa CRDB na wengine wanaofanya katika majengo yenye msongamano wa watu kutokuwa na wasiwasi kwani kikosi hicho kimejiandaa vilivyo kutegua hata mabomu yaliyotegwa na Osama mwenyewe wacha haya yanayotegwa na wafuasi wake. Hata baada ya maneno hayo wafanyakazi wa CRDB walionekana bado walikuwa na wasiwasi wa kurudi maofisini. Wachache walirudi maofisini japo hawakurudi kabisa mpaka siku ya tatu ya tukio.Kazi zote siku hiyo hazikufanyika kama kawaida kwani kila mahali walisikika wakisimulia jinsi walivyoruka kupitia madirishani, wengine walisikika wakiwacheka wenzao ambao BADALA YA KUTOKA NJE WALISIKIKA WAKILIA KWA SAUTI KUU."Yametufika yaliyowafika wamarekani". Itakumbukwa kuwa ni hivi majuzi tu watu zaidi ya 15000 walipoteza maisha yao huko marekani baada ya kulipuliwa wakiwa maofisini katika jengo moja huko New York lenye msongamano wa watu japo siyo kama CRDB Ya hapa Dar. Bado dunia nzima iko katika mshituko hasa baada ya kutangazwa kuwa waliofanya hayo ya Amerika ni Waislamu wanaodai haki yao ambayo wanahisi walinyanganywa na serikali ya amerika. Wenzetu wa CRDB walikuwa na kila sababu ya kuogopa kwani Tanzania tuna waislamu wenye machungu ya kuuliwa ndugu zao huko Zanzibar na serikali ya CCM. Isitoshe waislamu wanahisi kuwa kuna mpango wa serikali ya Amerika ikishirikiana na serikali ya CCM kuwanyanyasa na kuwanjima haki za msingi Waislamu wa Tanzania. Serikali ya Mkapa isipoyaangalia kwa makini na kuyatafutia uvumbuzi matatizo ya waislamu Tanzania, yanaweza kuifikisha Tanzania Pabaya.Tunaomba Mungu aepushe hayo kwa kuwapa moyo wakukubali kuwa CCM iko kimakosa madarakani, na iachie ngazi ili uchaguzi ufanywe upya. Ni juu yetu wananchi wa Tanzania kuwaambia akina Mkapa hayo.Tusipofanya hivyo tutajilaumu wenyewe yatakapotufika yaliyowafika waamerika. . Tatizo siyo Osama Bin Laden, bali tatizo ni Amerika. Osama na wote wanaodhaniwa kuwa maghaidi wakifa leo tatizo la ughaidi haliwezi kwisha duniani. Ughaidi ni matunda ya sera mbaya.Huwezi kuumaliza ughaidi bila kumaliza sera mbaya.Kila mtu anaweza kuwa ghaidi kulingana na mahali alipo na hasa kama anahisi kunyimwa haki zake za msingi. Amerika wana vita vya mafuta na waarabu.Hakuna dini hapo. Ni mafuta.Wasitudanganye kwamba wanapigwa vita vya kidini.Wamalize vita vyao huko Amerika na Uarabuni.Wasiingize dunia kwenye mzozo ambao wanaweza kuumaliza wenyewe.Hatuwataki Waamerika watusaidie kuutetea Ukristo.wasiutumie ukristo kulinda maslahi yao. Walokufa Amerika hawana hatia? Wana hatia kama walikubaliana na sera za serikali yao kuwanyanyasa wengine.Mimi ni Mkristo mwananchi wa Tanzania na sikubaliani na sera za serikali yetu kuwanyanyasa waislamu kwa sababu ya dini yao.Wakati umefika wananchi wa Amerika kupinga kwa nguvu zote sera za serikali yao.Wasipofanya hivyo wana hatia. Kwa nini mnawaogopa amerika? Sera zao ni mbaya na hamtaki kuwaambia wajirekebishe.Tatizo siyo walikufa wangapi,bali mauaji yataisha lini.Sera za Amerika ni mbaya,na hakuna anayewakemea. Amerika ilikosea kwa kiburi, waliowaua wakakosea, na sasa Amerika inataka kukosea tena.Makosa yataendelea mpaka lini? Maadui wa Amerika siyo waislamu kama wanavyotaka tuamini.Mungu hapendezwi na kiburi cha amerika.Wanasema ni vita ya waovu juu ya wema.Wanakosea.Waamerika siyo wema kama wanavyofikiri.Kama ni dini, ukristo hauhitaji kutetewa na Amerika Amerika ilijitengenezea maadui zake yenyewe kwa sera zake mbovu za kutaka kuitawala dunia ya Mungu bila idhini ya Muumbaji.Sasa wanaitaka dunia iwasaidie kupambana na maadui zao.Lazima wakubali kuwa wao siyo bora kuliko wanadamu wengine.Wajirekebishe kila upande, na hakuna atakayewadhuru. Paka ni mnyama wa kufugwa, na hana madhara kwa mwanadamu.Lakini mwanadamu akimpiga paka kwa sababu yoyote na awe amefunga mlango, paka anageuka chui na kuwa madhara kwa mwanadamu.Amerika imewapiga wengi duniani kwa sababu wanazozijua wao,na sasa inakuwa vigumu kujua ni nani aliyegeuka kuwa chui na kusababisha madhara makubwa namna hii kwa Waamerika. Hakuna SUPER POWER duniani.Ikiwa watu wanaweza kutumia visu kuziteka nyara ndege za Amerika na kuzitumia kama mabomu kuwalipua waamerika, basi tumefikia mahali pa kujiuliza kama tunahitaji silaha zote kali tulizojiwekea kujilinda.Wote tuko sawa. Tuliwaogopa bure kumbe kisu tu kinatosha.Sera za kuwanyanyasa wengine hazitalisaidia taifa lolote duniani.Sijui kama Mkapa anayasikia haya. Mkapa alisema atatumia nguvu za dola kuwaweka sawa wale anaowanyanyasa. Kama ni nguvu za dola Amerika ni zaidi ya TZ mara mia moja.Tunasubiri tuone atafika wapi na nguvu za dola.Haki kwa kila mtu ndiyo silaha kwa sasa.Bila haki, Nguvu za dola ni Bure.Waliouawa Zanzibar ni watu, ndugu zao wapo,wanaoendelea kupigwa marungu ya Polisi ni watu,na wanaowekwa ndani na kuteswa bure ni watu.Yakiwafika shingoni sijui watafanya nini.Tunao muda kuyarekebishe yasitufikishe pabaya Siungi mkono mauaji hasa ya raia wasio na hatia,au ya watu wasiohusika na mzozo wenyewe kama mabomu yaliyolipuliwa Nairobi na Dar,Lakini inapofikia kwamba wauaji ni watu walio tayari kufa, ni vizuri kujiuliza kile kinachowafikisha katika maamuzi ya namna hiyo, ili juhudi zifanywe kuepusha maafa kwa watu wasio na hatia. Inashangaza kuona kwamba hakuna kiongozi Afrika aliyepeleka misaada ya chakula na nguo huko Amerika.Ni wanadamu.Wakati huu wa maafa wanahitaji kila msaada. Mablanketi, kandambili, na watu wa kusaidia kuwatoa wale ambao bado wameshikiliwa kwenye mabaki ya kuta zilizowaangukia.Sote ni wanadamu tunahitajiana mmoja kwa mwingine. Wakati Mabomu yalipolipuka Nairobi na Dar,walisema Waafrika hawajajiandaa vya kutosha kutoa usaidizi wakati wa majanga.Sasa ni wazi kwamba hakuna anayeweza kujigamba kwamba yuko tayari kupambana na majanga .Polisi na wazima moto wa Amerika waliowahi kufika kwenye tukio walikufa wote. Zaidi ya 400. Kama ni vita Amerika imeshindwa vibaya.Sasa
wabadili sera zao ambazo zimechangia zaidi kusababisha haya.
Kusema watalipiza kisasi hawawezi.Waliokufa ni wengi zaidi
ya kulipiza kisasi. Kuchukua ndege na kuangusha mabomu Iraq
au pengine popote haitasaidia. Na mbaya zaidi wote wataonekana
wendawazimu.Wakubali kushindwa na wabadili sera zao sasa na
siyo baadaye.
|
||||||||||||
|
|
|
|